Basi Yoabu akaingia nyumbani kwa mfalme, akasema, Wewe leo umefedhehesha nyuso za watumishi wako wote, waliokuokoa leo roho yako, na roho za wanao, na za binti zako, na roho za wake zako, na roho za masuria wako;
Zaburi 34:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi, Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mgeukieni Mungu mpate kufurahi; nanyi hamtaaibishwa kamwe. Biblia Habari Njema - BHND Mgeukieni Mungu mpate kufurahi; nanyi hamtaaibishwa kamwe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mgeukieni Mungu mpate kufurahi; nanyi hamtaaibishwa kamwe. Neno: Bibilia Takatifu Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe. BIBLIA KISWAHILI Mwelekezeeni macho, mpate kufurahi, Na nyuso zenu hazitaaibishwa kamwe. |
Basi Yoabu akaingia nyumbani kwa mfalme, akasema, Wewe leo umefedhehesha nyuso za watumishi wako wote, waliokuokoa leo roho yako, na roho za wanao, na za binti zako, na roho za wake zako, na roho za masuria wako;
Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonesha wokovu wa Mungu.
Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.
Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Basi Daudi na watu wake, ambao walikuwa kama mia sita, wakaondoka na kutoka Keila, wakaenda popote walipoweza kwenda. Kisha Sauli akaambiwa ya kwamba Daudi amekimbia toka Keila; akauacha mpango wake.