Zaburi 34:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtukuzeni BWANA pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami, sote pamoja tulisifu jina lake. Biblia Habari Njema - BHND Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami, sote pamoja tulisifu jina lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami, sote pamoja tulisifu jina lake. Neno: Bibilia Takatifu Mtukuzeni Mwenyezi Mungu pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. Neno: Maandiko Matakatifu Mtukuzeni bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja. BIBLIA KISWAHILI Mtukuzeni BWANA pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja. |
Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini BWANA, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi BWANA, Mungu wa baba zao, wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudia BWANA, na mfalme naye.
Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.
Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake.
Washangilie na wakufurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima, BWANA ni Mkuu.
BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,
Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wagiriki waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.
kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama sikuzote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu.
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.