Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.
Zaburi 34:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA kutoka kwayo yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mateso ya mwadilifu ni mengi, lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote. Biblia Habari Njema - BHND Mateso ya mwadilifu ni mengi, lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mateso ya mwadilifu ni mengi, lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote. Neno: Bibilia Takatifu Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Mwenyezi Mungu humwokoa nayo yote, Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye haki ana mateso mengi, lakini bwana humwokoa nayo yote, BIBLIA KISWAHILI Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya na hayo yote. |
Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.
Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki, Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. Ndipo watakapotoa ng'ombe Juu ya madhabahu yako.
Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.
Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;