Zaburi 30:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Je, utapata faida gani nikifa na kushuka hadi kwa wafu? Je, mavumbi ya wafu yanaweza kukusifu? Je, yanaweza kusimulia uaminifu wako? Biblia Habari Njema - BHND “Je, utapata faida gani nikifa na kushuka hadi kwa wafu? Je, mavumbi ya wafu yanaweza kukusifu? Je, yanaweza kusimulia uaminifu wako? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Je, utapata faida gani nikifa na kushuka hadi kwa wafu? Je, mavumbi ya wafu yanaweza kukusifu? Je, yanaweza kusimulia uaminifu wako? Neno: Bibilia Takatifu “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu, katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako? Neno: Maandiko Matakatifu “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako? BIBLIA KISWAHILI Mna faida gani katika damu yangu Nishukapo Shimoni? Mavumbi yatakusifu? Yatautangaza uaminifu wako? |
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuutumainia uaminifu wako.