Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.
Zaburi 3:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uje ee Mwenyezi-Mungu! Niokoe ee Mungu wangu! Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote; wawavunja meno waovu wasinidhuru. Biblia Habari Njema - BHND Uje ee Mwenyezi-Mungu! Niokoe ee Mungu wangu! Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote; wawavunja meno waovu wasinidhuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uje ee Mwenyezi-Mungu! Niokoe ee Mungu wangu! Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote; wawavunja meno waovu wasinidhuru. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, amka! Niokoe, Ee Mungu wangu! Wapige adui zangu wote kwenye taya, vunja meno ya waovu. BIBLIA KISWAHILI BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki. |
Kwa maana vita vilienea huko juu ya uso wote wa nchi; na siku ile huo msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga.
Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumainia BWANA.
Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, uinuke. Uwapatilize mataifa yote; Usimrehemu hata mmoja wa wale wapangao maovu kwa hila.
BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Mbona unaurudisha mkono wako, Naam, mkono wako wa kulia, Uutoe kifuani mwako, Ukawaangamize kabisa.
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Ole wake yeye auambiaye mti, Amka; aliambiaye jiwe lisiloweza kusema, Ondoka! Je! Kitu hicho kitafundisha? Tazama, kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, wala hamna pumzi ndani yake kabisa.