Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Zaburi 3:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Biblia Habari Njema - BHND Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Neno: Bibilia Takatifu Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza. Neno: Maandiko Matakatifu Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana bwana hunitegemeza. BIBLIA KISWAHILI Nilijilaza na kulala usingizi, kisha nikaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. |
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala na hakuna atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.
Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakalilinda gereza.