Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Zaburi 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Biblia Habari Njema - BHND Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Neno: Bibilia Takatifu Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Ninamlilia bwana kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. BIBLIA KISWAHILI Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. |
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Nitumie nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata katika maskani yako.
Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.
Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.