Zaburi 25:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wenye upole atawaongoza katika haki, Wenye upole atawafundisha njia yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwaongoza wanyenyekevu katika uadilifu; naam, huwafundisha hao njia yake. Biblia Habari Njema - BHND Huwaongoza wanyenyekevu katika uadilifu; naam, huwafundisha hao njia yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwaongoza wanyenyekevu katika uadilifu; naam, huwafundisha hao njia yake. Neno: Bibilia Takatifu Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake. Neno: Maandiko Matakatifu Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake. BIBLIA KISWAHILI Wenye upole atawaongoza katika haki, Wenye upole atawafundisha njia yake. |
Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,
Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa heshima.
bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.