Zaburi 25:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watafanikiwa maishani mwao; Na wazawa wao wataimiliki nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima, na wazawa wake watamiliki nchi. Biblia Habari Njema - BHND Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima, na wazawa wake watamiliki nchi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima, na wazawa wake watamiliki nchi. Neno: Bibilia Takatifu Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi. BIBLIA KISWAHILI Watafanikiwa maishani mwao; Na wazawa wao wataimiliki nchi. |
Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako Ulizowawekea wakuchao; Ulizowatendea wakukimbiliao Mbele ya wanadamu!
Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.
nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao;
BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.
Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake.
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Akamnena Benyamini, Mpenzi wa BWANA atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake.
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme uongo.
Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.