Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako, Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
Zaburi 25:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, unisamehe kosa langu kwani ni kubwa. Biblia Habari Njema - BHND Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, unisamehe kosa langu kwani ni kubwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, unisamehe kosa langu kwani ni kubwa. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi. |
Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako, Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.
Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie, Kwa ajili ya utukufu wa jina lako. Utuokoe, utusamehe dhambi zetu, Kwa ajili ya jina lako.
mwenye kuwaonea huruma watu maelfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali.
Ijapokuwa maovu yetu yanatushuhudia, lakini utende wewe kwa ajili ya jina lako, Ee BWANA, maana kurudi nyuma kwetu ni kwingi; tumekutenda dhambi.
Lakini nilitenda kwa ajili ya jina langu, ili lisitiwe unajisi mbele ya macho ya mataifa, ambao walikaa pamoja nao, ambao machoni pao nilijidhihirisha kwao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mlikoenda.
Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.