Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Zaburi 24:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari; aliisimika imara juu ya mito ya maji. Biblia Habari Njema - BHND Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari; aliisimika imara juu ya mito ya maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari; aliisimika imara juu ya mito ya maji. Neno: Bibilia Takatifu maana aliiwekea misingi yake baharini, na kuifanya imara juu ya maji. Neno: Maandiko Matakatifu maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji. BIBLIA KISWAHILI Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. |
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.
Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.