Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
Zaburi 24:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu. Biblia Habari Njema - BHND Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu. Neno: Bibilia Takatifu Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni; yeye ndiye Mfalme wa utukufu. Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni bwana Mwenye Nguvu Zote; yeye ndiye Mfalme wa utukufu. BIBLIA KISWAHILI Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu. |
Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko katika mkono wake wa kulia, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba?
tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;