Zaburi 22:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wazawa wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za BWANA, Kwa kizazi kitakachokuja, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Vizazi vijavyo vitamtumikia; watu watavisimulia habari za Mwenyezi-Mungu, Biblia Habari Njema - BHND Vizazi vijavyo vitamtumikia; watu watavisimulia habari za Mwenyezi-Mungu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Vizazi vijavyo vitamtumikia; watu watavisimulia habari za Mwenyezi-Mungu, Neno: Bibilia Takatifu Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. Neno: Maandiko Matakatifu Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. BIBLIA KISWAHILI Wazao wake watamtumikia. Zitasimuliwa habari za BWANA, Kwa kizazi kitakachokuja, |
Hapo ndipo waovu watakaposhikwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
Lakini BWANA aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;
wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Abrahamu watoto.
Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;