BWANA, utatazama hadi lini? Uiokoe nafsi yangu kutoka kwa maangamizi yao, Na maisha yangu kutoka kwa wanasimba.
Zaburi 22:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniokoe kinywani mwa simba; iokoe nafsi yangu dhaifu toka pembe za nyati hao. Biblia Habari Njema - BHND Uniokoe kinywani mwa simba; iokoe nafsi yangu dhaifu toka pembe za nyati hao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniokoe kinywani mwa simba; iokoe nafsi yangu dhaifu toka pembe za nyati hao. Neno: Bibilia Takatifu Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za nyati. Neno: Maandiko Matakatifu Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. BIBLIA KISWAHILI Kinywani mwa simba uniokoe; Naam, toka pembe za nyati umenijibu. |
BWANA, utatazama hadi lini? Uiokoe nafsi yangu kutoka kwa maangamizi yao, Na maisha yangu kutoka kwa wanasimba.
Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.
Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.
Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba.
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.