Zaburi 22:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadui wengi wanizunguka kama fahali; wamenisonga kama fahali wakali wa Bashani! Biblia Habari Njema - BHND Maadui wengi wanizunguka kama fahali; wamenisonga kama fahali wakali wa Bashani! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadui wengi wanizunguka kama fahali; wamenisonga kama fahali wakali wa Bashani! Neno: Bibilia Takatifu Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira. Neno: Maandiko Matakatifu Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira. BIBLIA KISWAHILI Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; |
Waaibike na wafedheheke, Wote wanaotaka kuniua. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
Mkemee mnyama wa mafunjoni; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita.
Waaibike, wafedheheke, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu.
Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;
Mtakula nyama yao walio hodari, na kunywa damu ya wakuu wa dunia, ya kondoo dume na ya wana-kondoo, na ya mbuzi, na ya ng'ombe, wote na wanono wa Bashani.
Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,