Zaburi 21:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA, Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa mfalme anamtumaini bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA, Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika. |
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.