Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.
Zaburi 21:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alikuomba maisha nawe ukampa; ulimpa maisha marefu milele na milele. Biblia Habari Njema - BHND Alikuomba maisha nawe ukampa; ulimpa maisha marefu milele na milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alikuomba maisha nawe ukampa; ulimpa maisha marefu milele na milele. Neno: Bibilia Takatifu Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele. Neno: Maandiko Matakatifu Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele. BIBLIA KISWAHILI Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. |
Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa BWANA.
Ila mfalme Sulemani atakuwa amebarikiwa, na kiti cha enzi cha Daudi kitathibitika mbele za BWANA hata milele.
Ndipo akamleta nje mwana wa mfalme, akamvika taji, na kumpa ushuhuda; wakamfanya mfalme, wakamtia mafuta; wakapiga makofi, wakasema, Mfalme na aishi.
Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.
Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.
Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atakuwa na heshima ya kifalme; na ataketi na kutawala; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na maelewano yenye amani yatakuwa kati ya hao wawili.
na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.