Zaburi 21:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako, anafurahi mno kwa msaada uliompa. Biblia Habari Njema - BHND Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako, anafurahi mno kwa msaada uliompa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mfalme ashangilia, ee Mwenyezi-Mungu, kwa nguvu yako, anafurahi mno kwa msaada uliompa. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi furaha yake ilivyo kuu kwa ushindi unaompa! Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa! BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. |
BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.
Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.
Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.