vitu hivi vyote, Ee mfalme, mimi Arauna nakupa wewe mfalme. Kisha Arauna akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na akukubali.
Zaburi 20:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kukutimizia mipango yako yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akujalie unayotamani moyoni mwako, aifanikishe mipango yako yote. Biblia Habari Njema - BHND Akujalie unayotamani moyoni mwako, aifanikishe mipango yako yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akujalie unayotamani moyoni mwako, aifanikishe mipango yako yote. Neno: Bibilia Takatifu Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote. Neno: Maandiko Matakatifu Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote. BIBLIA KISWAHILI Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kukutimizia mipango yako yote. |
vitu hivi vyote, Ee mfalme, mimi Arauna nakupa wewe mfalme. Kisha Arauna akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na akukubali.
Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichokitaka na zaidi ya vile alivyomletea mfalme. Basi akarudi, akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Haja ya mwenye haki ni kupata mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu huishia katika ghadhabu.
Nami nilijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nilisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu.
Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.
Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.