Zaburi 20:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akutumie msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake; akutegemeze kutoka mlima Siyoni. Biblia Habari Njema - BHND Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake; akutegemeze kutoka mlima Siyoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akupelekee msaada kutoka hekaluni mwake; akutegemeze kutoka mlima Siyoni. Neno: Bibilia Takatifu Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni. Neno: Maandiko Matakatifu Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni. BIBLIA KISWAHILI Akutumie msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. |
Wakaliingiza sanduku la BWANA, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.
Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu.
Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.