Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 20:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mwenyezi-Mungu akujibu uwapo taabuni; jina la Mungu wa Yakobo likulinde.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

BWANA akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 20:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.


Nijapopitia katika shida, Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu, Unaunyosha mkono wako, Na mkono wako wa kulia unaniokoa.


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Heri amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu.


Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.


Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.


Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai kitu.


Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.


Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.


Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa kutoka kwayo.


Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;