Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
Zaburi 2:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema: Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, anawakaripia kwa ghadhabu, na kuwatisha kwa hasira, akisema: Biblia Habari Njema - BHND Kisha, anawakaripia kwa ghadhabu, na kuwatisha kwa hasira, akisema: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, anawakaripia kwa ghadhabu, na kuwatisha kwa hasira, akisema: Neno: Bibilia Takatifu Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, Neno: Maandiko Matakatifu Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, BIBLIA KISWAHILI Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake, akisema: |
Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa BWANA, Na ya hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.
Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawateketeza.
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.
Sauti ya fujo itokayo mjini! Sauti itokayo hekaluni! Sauti ya BWANA awalipaye adui zake adhabu!
Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.
Basi yule mfalme akaghadhibika; akatuma majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili kwa upanga huo awapige mataifa. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.