Tamko alilolitamka BWANA katika habari zake ndilo hili, Bikira, binti Sayuni, amekudharau, na kukudhihaki sana; binti Yerusalemu ametikisa kichwa chake juu yako.
Zaburi 2:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni, anawacheka na kuwadhihaki. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni, anawacheka na kuwadhihaki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu atawalaye juu mbinguni, anawacheka na kuwadhihaki. Neno: Bibilia Takatifu Yeye anayetawala mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. BIBLIA KISWAHILI Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka. |
Tamko alilolitamka BWANA katika habari zake ndilo hili, Bikira, binti Sayuni, amekudharau, na kukudhihaki sana; binti Yerusalemu ametikisa kichwa chake juu yako.
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.
Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu, Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru. Umewatia aibu, Kwa sababu MUNGU amewadharau.
Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?