Zaburi 2:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima, Enyi watawala wa dunia, mwaonywa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sasa enyi wafalme, tumieni busara; sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia. Biblia Habari Njema - BHND Sasa enyi wafalme, tumieni busara; sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sasa enyi wafalme, tumieni busara; sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. BIBLIA KISWAHILI Na sasa, enyi wafalme, iweni na hekima, Enyi watawala wa dunia, mwaonywa. |
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
ndivyo atakavyowastusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.
Uonyeke, Ee Yerusalemu, nafsi yangu, isije ikafarakana nawe; nisije nikakufanya ukiwa, nchi isiyokaliwa na watu.
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, BWANA wa majeshi, mvua haitanyesha kwao.