Zaburi 19:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchana waupasha habari mchana ufuatao, usiku waufahamisha usiku ufuatao. Biblia Habari Njema - BHND Mchana waupasha habari mchana ufuatao, usiku waufahamisha usiku ufuatao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchana waupasha habari mchana ufuatao, usiku waufahamisha usiku ufuatao. Neno: Bibilia Takatifu Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. Neno: Maandiko Matakatifu Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa. BIBLIA KISWAHILI Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. |
Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.