Zaburi 19:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe? Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua. Biblia Habari Njema - BHND Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe? Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini nani aonaye makosa yake mwenyewe? Ee Mungu, niepushe na makosa nisiyoyajua. Neno: Bibilia Takatifu Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. BIBLIA KISWAHILI Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri. |
Kwa maana mabaya yasiyohesabika Yamenizunguka mimi. Maovu yangu yamenipata, Wala siwezi kuona. Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu, Nami nimevunjika moyo.
BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa vibao vya mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe.
Kila anayelidharau neno hujiletea uharibifu; Bali yeye anayeiogopa amri atapewa thawabu.
Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.
Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele!
Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto.
Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi walizozitenda hao watu bila kujua.
bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.