Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.
Zaburi 18:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wageni nao walitepetea, Walitoka katika ngome zao wakitetemeka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wageni walikufa moyo; wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka. Biblia Habari Njema - BHND Wageni walikufa moyo; wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wageni walikufa moyo; wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka. Neno: Bibilia Takatifu Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. Neno: Maandiko Matakatifu Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka. BIBLIA KISWAHILI Wageni nao walitepetea, Walitoka katika ngome zao wakitetemeka. |
Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.
Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.
Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika.
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.
wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwenye hasira ya Mwana-kondoo.