Zaburi 18:41 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita BWANA lakini hakuwajibu, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipiga yowe lakini hapakuwa na wa kuwaokoa; walimlilia Mwenyezi-Mungu lakini hakuwajibu. Biblia Habari Njema - BHND Walipiga yowe lakini hapakuwa na wa kuwaokoa; walimlilia Mwenyezi-Mungu lakini hakuwajibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipiga yowe lakini hapakuwa na wa kuwaokoa; walimlilia Mwenyezi-Mungu lakini hakuwajibu. Neno: Bibilia Takatifu Walipiga yowe, lakini hapakuwa na mtu wa kuwaokoa; walimlilia Mwenyezi Mungu, lakini hakuwajibu. Neno: Maandiko Matakatifu Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa; walimlilia bwana, lakini hakuwajibu. BIBLIA KISWAHILI Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita BWANA lakini hakuwajibu, |
Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitaleta mabaya juu yao, ambayo hawataweza kuyakimbia; nao watanililia, lakini sitawasikiliza.
Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni.
Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitawaonea huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.
Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi.
Ndipo watakapomwomba BWANA, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao.
Ikawa kama wakati nilipowaita, wasitake kunisikiliza; basi, nao wataniita, wala sitasikiliza, asema BWANA wa majeshi.
Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
Baadaye Yoshua akawapiga, na kuwaua, akawatundika katika miti mitano; nao wakawa wametundikwa katika hiyo miti hadi jioni.