Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Zaburi 18:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kamba za kifo zilinizingira, mawimbi ya maangamizi yalinivamia; Biblia Habari Njema - BHND Kamba za kifo zilinizingira, mawimbi ya maangamizi yalinivamia; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kamba za kifo zilinizingira, mawimbi ya maangamizi yalinivamia; Neno: Bibilia Takatifu Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. Neno: Maandiko Matakatifu Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. BIBLIA KISWAHILI Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. |
Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.
Nao walipoanza kuimba na kusifu, BWANA akaweka waviziao juu ya Waamoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja kushambulia Yuda; nao wakapigwa.
Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenidunga mikono na miguu.
Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.
Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka kama kumkamata mnyang'anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku niliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.
Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni; mara milango ikafungwa.
Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,