Zaburi 18:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu ndiye anijaliaye nguvu kila upande; ndiye anayeifanya salama njia yangu. Biblia Habari Njema - BHND Mungu ndiye anijaliaye nguvu kila upande; ndiye anayeifanya salama njia yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu ndiye anijaliaye nguvu kila upande; ndiye anayeifanya salama njia yangu. Neno: Bibilia Takatifu Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. Neno: Maandiko Matakatifu Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. BIBLIA KISWAHILI Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. |
BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, ukuu na nguvu, kama mavazi ya kifalme. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuambia haya zamani na kuyatangaza? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakuimarisha ijapokuwa hukunijua;
Si kwamba tunatosha sisi wenyewe kufikiri kuwa neno lolote ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu.
Baada ya hayo kulikuwa na vita tena; naye Daudi akatoka, naye akapigana na Wafilisti, naye akawaua kwa uuaji mkuu; nao wakakimbia mbele yake.