Zaburi 18:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana Wewe wawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wenye majivuno huwaporomosha. Biblia Habari Njema - BHND Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wenye majivuno huwaporomosha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wenye majivuno huwaporomosha. Neno: Bibilia Takatifu Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi. Neno: Maandiko Matakatifu Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi. BIBLIA KISWAHILI Maana Wewe wawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. |
Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Mungu Hatapatiliza. Mawazo yake yote ni, Hakuna Mungu;
Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.
Inuka, Ee BWANA, umkabili, umwangushe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi yangu na mtu mbaya.
Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitamwadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.
Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?