Zaburi 18:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu; lakini mkatili kwa watu walio waovu. Biblia Habari Njema - BHND Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu; lakini mkatili kwa watu walio waovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu; lakini mkatili kwa watu walio waovu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa aliye mtakatifu, unajionesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionesha kuwa mkaidi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi. BIBLIA KISWAHILI Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi. |
Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya BWANA imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu?
dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Mgiriki pia;
Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nilisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau nitawadharau.