Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na mkononi mwa Sauli;
Zaburi 18:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walinivamia nilipokuwa taabuni, lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu. Biblia Habari Njema - BHND Walinivamia nilipokuwa taabuni, lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walinivamia nilipokuwa taabuni, lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu. Neno: Bibilia Takatifu Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Mwenyezi Mungu alikuwa msaada wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini bwana alikuwa msaada wangu. BIBLIA KISWAHILI Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu. |
Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na mkononi mwa Sauli;
Nijapopitia katika shida, Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu, Unaunyosha mkono wako, Na mkono wako wa kulia unaniokoa.
Nami nitaimba juu ya nguvu zako, Nitaimba kwa furaha juu ya fadhili zako asubuhi. Maana umekuwa ngome yangu, na kimbilio wakati wa mateso yangu.
Nami nitawatawanya mbele ya adui, kama kwa upepo wa mashariki; nami nitaviangalia visogo vyao, wala si nyuso zao, siku ya msiba wao.
Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.
Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.