Zaburi 17:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haki yangu na ije kutoka kwako, kwani wewe wajua jambo lililo la haki. Biblia Habari Njema - BHND Haki yangu na ije kutoka kwako, kwani wewe wajua jambo lililo la haki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haki yangu na ije kutoka kwako, kwani wewe wajua jambo lililo la haki. Neno: Bibilia Takatifu Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki. Neno: Maandiko Matakatifu Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki. BIBLIA KISWAHILI Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya adili. |
Lakini ninyi mwasema, Njia ya Bwana si sawa. Sikilizeni sasa, Enyi nyumba ya Israeli; Je! Njia yangu siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa?
Lakini nyumba ya Israeli husema, Njia ya Bwana si sawa. Ee nyumba ya Israeli, je! Njia zangu sizo zilizo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa?
Walakini wana wa watu wako husema, Njia ya Bwana si sawa; lakini watu hao, njia yao si sawa.
Lakini ninyi husema, Njia ya Bwana si sawa. Ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu ninyi; kila mtu kwa kadiri ya njia zake.
Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;