Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Zaburi 16:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu. Biblia Habari Njema - BHND Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu. Neno: Bibilia Takatifu Kuhusu watakatifu walio duniani, hao ndio wenye fahari, na ninapendezwa nao. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. BIBLIA KISWAHILI Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. |
Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
Mwimbieni BWANA zaburi, Enyi watauwa wake. Na kutoa shukrani. Kwa kukumbuka utakatifu wake.
Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefziba; na nchi yako Beula; kwa kuwa BWANA anakufurahia, na nchi yako itaolewa.
Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.
Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa watakatifu walioko [Efeso] wanaomwamini Kristo Yesu.
Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyasisitizie sana, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Mambo hayo ni mazuri sana, tena yana manufaa kwa wanadamu.
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.