Zaburi 16:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; Sina wema ila utokao kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Namwambia Mungu: “Wewe u Bwana wangu; sina jema lolote ila wewe.” Biblia Habari Njema - BHND Namwambia Mungu: “Wewe u Bwana wangu; sina jema lolote ila wewe.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Namwambia Mungu: “Wewe u Bwana wangu; sina jema lolote ila wewe.” Neno: Bibilia Takatifu Nilimwambia Mwenyezi Mungu, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” Neno: Maandiko Matakatifu Nilimwambia bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” BIBLIA KISWAHILI Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; Sina wema ila utokao kwako. |
Ee, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.
Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.
Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.
Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.