Zaburi 16:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unilinde ee Mungu; maana kwako nakimbilia usalama. Biblia Habari Njema - BHND Unilinde ee Mungu; maana kwako nakimbilia usalama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unilinde ee Mungu; maana kwako nakimbilia usalama. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. BIBLIA KISWAHILI Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe. |
Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.
Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,
Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.