Tena akamwasi mfalme Nebukadneza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie BWANA, Mungu wa Israeli.
Zaburi 15:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ni mtu anayewadharau wafisadi, lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu; ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara; Biblia Habari Njema - BHND ni mtu anayewadharau wafisadi, lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu; ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ni mtu anayewadharau wafisadi, lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu; ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara; Neno: Bibilia Takatifu ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia. Neno: Maandiko Matakatifu ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia. BIBLIA KISWAHILI Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake. |
Tena akamwasi mfalme Nebukadneza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie BWANA, Mungu wa Israeli.
Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.
Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
Na Paulo alipokuwa akitoa hoja zake kuhusu haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja, Feliki akaingiwa na hofu na kusema, Sasa nenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.
nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi; basi tulipoabiri wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.
Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana tunawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.
Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.