Zaburi 15:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu? Biblia Habari Njema - BHND Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu? Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? Neno: Maandiko Matakatifu bwana, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? BIBLIA KISWAHILI BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu? |
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.
Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu elfu mia moja na arubaini na nne pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.