Zaburi 148:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msifuni, enyi mbingu za juu, na maji yaliyo juu ya mbingu. Biblia Habari Njema - BHND Msifuni, enyi mbingu za juu, na maji yaliyo juu ya mbingu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msifuni, enyi mbingu za juu, na maji yaliyo juu ya mbingu. Neno: Bibilia Takatifu Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga. Neno: Maandiko Matakatifu Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga. BIBLIA KISWAHILI Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. |
Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
Lakini Mungu je? Hakika atakaa juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!
Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote.
Ezra akasema, Wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako; wewe ulifanya mbingu, mbingu za mbingu, pamoja na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, bahari na vitu vyote vilivyomo, nawe unavihifadhi vitu hivi vyote; na jeshi la mbinguni lakusujudu wewe.
Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,
Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Tazama, mbingu ni mali ya BWANA, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.