Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Zaburi 148:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msifuni, enyi jua na mwezi, msifuni, enyi nyota zote zingaazo. Biblia Habari Njema - BHND Msifuni, enyi jua na mwezi, msifuni, enyi nyota zote zingaazo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msifuni, enyi jua na mwezi, msifuni, enyi nyota zote zing'aazo. Neno: Bibilia Takatifu Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zinazong’aa. Neno: Maandiko Matakatifu Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zing’aazo. BIBLIA KISWAHILI Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga. |
Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa joto, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
BWANA asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake,
tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.