Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.
Zaburi 147:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwapa wanyama chakula chao, na kuwalisha makinda ya kunguru yanapolia. Biblia Habari Njema - BHND Huwapa wanyama chakula chao, na kuwalisha makinda ya kunguru yanapolia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwapa wanyama chakula chao, na kuwalisha makinda ya kunguru yanapolia. Neno: Bibilia Takatifu Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia. Neno: Maandiko Matakatifu Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia. BIBLIA KISWAHILI Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao. |
Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.
Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!