Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Zaburi 147:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari; Biblia Habari Njema - BHND Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye hataki nguvu za farasi, wala hapendezwi na ushujaa wa askari; Neno: Bibilia Takatifu Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya shujaa. Neno: Maandiko Matakatifu Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu. BIBLIA KISWAHILI Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji. |
Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!
Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.
Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.