Akasema, BWANA asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya uwanjani mwa kupuria, au ya shinikizoni?
Zaburi 146:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msiwategemee wakuu wa dunia; hao ni binadamu tu, hawawezi kuokoa. Biblia Habari Njema - BHND Msiwategemee wakuu wa dunia; hao ni binadamu tu, hawawezi kuokoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msiwategemee wakuu wa dunia; hao ni binadamu tu, hawawezi kuokoa. Neno: Bibilia Takatifu Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa. Neno: Maandiko Matakatifu Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa. BIBLIA KISWAHILI Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. |
Akasema, BWANA asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya uwanjani mwa kupuria, au ya shinikizoni?
Wakati huo Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea BWANA, Mungu wako, kwa hiyo limekutoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako.
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake iko katika mianzi ya pua yake; kwa maana wanafaa kitu gani?
Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ule msumari uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana BWANA amesema haya.
Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi wao ni nyama wala si roho; na BWANA atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wataangamia wote pamoja.
Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.