na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Zaburi 145:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu, nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake. Biblia Habari Njema - BHND Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu, nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Viumbe vyote vinakutazama kwa hamu, nawe wavipa chakula chao kwa wakati wake. Neno: Bibilia Takatifu Macho ya watu wote yanakutazama, nawe huwapa chakula chao wakati wake. Neno: Maandiko Matakatifu Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake. BIBLIA KISWAHILI Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao kwa wakati wake. |
na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Msiogope, enyi wanyama wa porini; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake.
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kuliko hao?
Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.