Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Zaburi 142:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nikiangalia upande wa kulia na kungojea, naona hakuna mtu wa kunisaidia; sina tena mahali pa kukimbilia, hakuna mtu anayenijali. Biblia Habari Njema - BHND Nikiangalia upande wa kulia na kungojea, naona hakuna mtu wa kunisaidia; sina tena mahali pa kukimbilia, hakuna mtu anayenijali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nikiangalia upande wa kulia na kungojea, naona hakuna mtu wa kunisaidia; sina tena mahali pa kukimbilia, hakuna mtu anayenijali. Neno: Bibilia Takatifu Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama kuume kwangu na uone, hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. Sina kimbilio, hakuna anayejali maisha yangu. BIBLIA KISWAHILI Utazame mkono wangu wa kuume ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho. |
Lakini macho ya waovu yataingia kiwi, Nao hawatakuwa na njia ya kukimbilia, Na matumaini yao yatakuwa ni kutoa roho.
Kwa sababu ya watesi wangu nimelaumiwa, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Wanaoniona njiani wananikimbia.
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Kilio na kisikiwe kitokacho katika nyumba zao, hapo utakapoleta kikosi juu yao kwa ghafla; kwa maana wamenichimbia shimo waninase, nao wameifichia miguu yangu mitego.
Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.
Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
Katika utetezi wangu wa kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.
Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kunihusu, asinitafute tena kote mipakani mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake.