Zaburi 142:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ninapokaribia kukata tamaa kabisa, yeye yupo, anajua mwenendo wangu. Maadui wamenitegea mitego njiani mwangu. Biblia Habari Njema - BHND Ninapokaribia kukata tamaa kabisa, yeye yupo, anajua mwenendo wangu. Maadui wamenitegea mitego njiani mwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ninapokaribia kukata tamaa kabisa, yeye yupo, anajua mwenendo wangu. Maadui wamenitegea mitego njiani mwangu. Neno: Bibilia Takatifu Roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita, watu wameniwekea mtego. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego. BIBLIA KISWAHILI Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu; Katika njia niendayo wamenifichia mtego. |
Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.
Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.
Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Kilio na kisikiwe kitokacho katika nyumba zao, hapo utakapoleta kikosi juu yao kwa ghafla; kwa maana wamenichimbia shimo waninase, nao wameifichia miguu yangu mitego.
Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.