Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Zaburi 142:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Namwekea malalamiko yangu, namweleza taabu zangu. Biblia Habari Njema - BHND Namwekea malalamiko yangu, namweleza taabu zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Namwekea malalamiko yangu, namweleza taabu zangu. Neno: Bibilia Takatifu Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu. Neno: Maandiko Matakatifu Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu. BIBLIA KISWAHILI Nitafunua mbele zake malalamiko yangu, Shida yangu nitaitangaza mbele zake. |
Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;