Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Zaburi 142:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Namlilia Mwenyezi-Mungu kwa sauti, namsihi Mwenyezi-Mungu kwa sauti yangu. Biblia Habari Njema - BHND Namlilia Mwenyezi-Mungu kwa sauti, namsihi Mwenyezi-Mungu kwa sauti yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Namlilia Mwenyezi-Mungu kwa sauti, namsihi Mwenyezi-Mungu kwa sauti yangu. Neno: Bibilia Takatifu Namlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti, napaza sauti yangu kwa Mwenyezi Mungu anihurumie. Neno: Maandiko Matakatifu Namlilia bwana kwa sauti, nainua sauti yangu kwa bwana anihurumie. BIBLIA KISWAHILI Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA, Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua. |
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.
(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizungukazunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.
Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kwenda haja. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana.
Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yoyote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.