Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako.
Zaburi 141:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache bila kinga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bali mimi nakutegemea, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; ninakimbilia usalama kwako, usiniache hatarini. Biblia Habari Njema - BHND Bali mimi nakutegemea, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; ninakimbilia usalama kwako, usiniache hatarini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bali mimi nakutegemea, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; ninakimbilia usalama kwako, usiniache hatarini. Neno: Bibilia Takatifu Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee bwana Mwenyezi, ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. BIBLIA KISWAHILI Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache bila kinga. |
Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako.
BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu?
Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, BWANA, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.